24 Februari 2018

Mwanamke anusurika kifo kwa kushambuliwa na samaki aina ya PAPA


Mwanamke mmoja nchini  Australia mwenye umri wa miaka 55 amenusurika kifo jioni ya jana February 23, 2018 baada ya kushambuliwa na papa wakati anaogelea baharini katika eneo la Sydney Kusini-Mashariki.
Inaaminika kuwa papa huyo alikuwa na urefu wa kati ya mita 2.7 hadi 3.2. Mwanamke huyo alikimbizwa hospitali ya St George kupatiwa matibabu ambapo alikuwa amejeruhiwa kwenye mguu wake wa kulia.
Wakazi mbalimbali wa eneo hilo waliliambia shirika la utangazaji nchini Australia la ABCkuwa tukio hilo limewashtua kwani halijatokea kipindi cha zaidi ya miaka 25 hivyo ni la ajabu.
Mwanamke huyo amefanyiwa upasuaji na afya yake imeanza kuimarika

16 Februari 2018

Kisa cha kwanza cha mwanamume aliyejibadilisha jinsia 'kumnyonyesha mtoto'


Mwanamume aliyejibadilisha jinis na kuwa mwanamke amefanikiwa kumyonyesha mtoto katika kisa cha kwanza cha iana yake kuwahi kushuhudiwa, watafiti wanasema.
Mwanmke huyo mwenye umri wa miaka 30 alitaka kumnyonyesha mtoto baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo, hayoni kwa mujibu wa wa jarida la afya la watu waliojibadili jinsia.
Alifanikiwa kunyonyesha baada ya kumeza dawa na kukamua maziwa, ripotihiyo inasema kutoka nchini Marekani.
Mtaalamu wa Marekani anasema utafiti huo huenda ukachangia visa zaidi vya wanaume walijibadilisha jinsia kuwa wanawake kunyonyesha watoto.
Mwanamke huyo aliyekuwa anapokea matibabu ya kubadili homoni zake mwilini kwa muda wa miaka 6, lakini hajafanyiwa upasuaji kubadili sehemu zake za siri, wakati alipowaomba madaktari wamsaidie atimize lengo lake la kumnyonyesha mtoto.
Bibi awa mama Uingereza
Mama anayemnunulia heroine mwanawe
Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, madakatari walimpadawa za miezi mitatu unusu kumsaidia kupata maziwa, kwa kawaida dawa hizo hupewa wanawake waliowaasili watoto au waliojipatia watoto kupitia wanawake wanobeba mimba kibiashara kuwaisaidia wasioweza kuzaa.
Dawa hizo husisimua homoni mwilini kushinikiza kutoa maziwa na kuzuia homoni za kiume na pia alihitajika kukamua maziwa yake.
Na mtokeo yake, yalimsababisha mwanamke huyo kuweza kupata maziwa kiasi.
Watafiti wanasema mtoto huyo alikunywa maziwa hayo tuu kwa wiki zake sita za uhai, wakatiambapo ukuwaji wake, ulaji na uwendaji haja wake ulikuwa unaendelea kama kawaida.
Baada ya hapa, mtoto alianza kupewa maziwa ya mkebe kwasababu maziwa yalianza kupungua.
Mtoto huyo sasa ana miezi sita na anendelea kunyonya kama sehemu ya lishe yake, wahiriri wa utafiti huo wanasema.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Watafiti wamesema utafiti zaidi unahitajika kubaini matibabu halisi ya wanaume wanaojibadili jinsia kuwa wanawake wanaotaka kunyonyesha
Dkt Channa Jayasena, mhadhiri mkuu katika chuo cha Imperial College anayejishughulisha na masuala ya uzazi amesema, utafiti huo ni 'hatua nzuri'.
Amesema ameshasikia visa kadhaa nchini Uingereza vya wanaume waliogeuka kuwa wanawake wanasaidiwa kunyonyesha, lakini mpaka sasa hakuna ripoti iliyochapishwa.
Amesema:"Tunachohiaji kufanya nikuvikusanya visa hivi na tusaidiane ki mawazo, tutafute mbinu muafaka kuwasaidia kunyonyesha bila ya kuwadhuru ki afya."
Watafiti wanasema haijabainika wazi iwapo dawa zote zinzotumika zinahitajika kufanikisha wazazi hao kuwawezesha kunyonyesha.
Wamesema uchunguzi zaidi unahitajika kubaini matibabu halisi ya wanaume wanaojibadili jinsia kuwa wanawake wanaotaka kunyonyesha.

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728