04 Machi 2021

PATA UFAHAMU: TUNDA NA JANI LA MPERA.


Mperera ni mti maarufu kwa matunda yake, ila wengi wetu huenda hatujui faida zinginezo; zinatokana na mti huu wa matunda, aliyotujalia Mungu Baba kama ilivyo katika mapenzi Yake.
IMEANDIKWA: Mungu akasema,
“Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;”.... 📖» MWANZO 1:29
KIPEKEE; Matunda na majani ya mti wa mpera vina vitamini C kwa wingi, huku ikiambatana na madini ya potassium kwa asilimia chache 15%.
Kutokana na sifa tajwa, basi fahamu kuwa iwapo ukikosa tunda la pera unaweza kutumia majani yake kama m’badala; ili kujipatia faida za asili, zinazotokana na mpera kwa faida ya afya ya mwili wako. Nami nimekuja nikudokeze japo kwa ufupi, faida za matunda na majani ya mpera; iwapo utabarikiwa kuwa nayo karibu.
Kutokana na sifa ya vitamini C & madini tajwa yaliyomo ndani yake, tunda la pera pamoja na majani yake; yanasaidia sana ustawi na uimara wa mifupa ya mwili wako, huku yakiwa pia na uwezo/neema ya kuchochea pia kinga ya mwili
Ila tambua katika tunda lake, utapata madini ya potassium zaidi kuliko vitamini C; hii ni kwa sababu ya mbegu za mpera, zimebeba madini husika kwa asilimia kubwa kuliko vitamini C. Ni
majani yake ndiyo yaliyobeba VITAMINI C zaidi.
JE! UMEWAHI KUTUMIA MAJANI YA MPERA KAMA M’BADALA YA MAJANI YA CHAI !?
Majani ya mpera ukiyafanya kuwa kiungo kikuu cha chai, basi utakuwa umeji-tengenezea dawa kwa jina la chai; inayo shughulika na kuondoa mafuta yanayoganda mwilini (cholesterol), bila kusahau na kusafisha sumu zinginezo mwilini.
FAIDA ZA ZIADA NI:
~Inaimarisha afya ya ngozi.
~Inaponya maumivu ya tumbo na kuharisha.
~Inasaidia kuweka uwiano wa sukari mwilini.
~Inaboresha afya ya uoni kwenye macho (B3).
~Inasaidia kupunguza uzito mkubwa (obesity).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728