Katika taarifa yake,limesema kuwa kile lilichozuia ni mikutano ya hadhara ambayo lilihisi itavuruga hali ya usalama
Hivyobasi jeshi hilo sasa limewataka wananchi kupuuza taarifa kuwa wao walizuia mikutano ya kisiasa.
"Jeshi
la Polisi linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia
tarehe
07/06/2016 hadi hapo hali ya kiusalama itakapotengemaa."
Kulingana
na nukuu hiyo jeshi hilo linasema kuwa hakuna sehemu yoyote iliyopiga
marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya kisiasa
inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.
Jeshi
hilo limetoa mfano wa Chama cha CUF kilichotangaza kuwa kimepanga
kufanya mkutano mkuu kujaza nafasi ya Mwenyekiti wao wa Taifa tarehe 21
Agosti, 2016,na ambao Polisi hawakujitokeza kuuzuia.
10 Julai 2016
Polisi wakanusha kuzuia mikutano ya kisiasa TZ
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni