Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari
amekaribisha Umoja wa mataifa kujadiliana na Boko Haram katika kutafuta
kumaliza uasi wa miaka 7 wa wanamgambo hao wa kiisalmu na kuwaokoa zaidi
ya wasichana 200 wa shule waliotekwa kutoka Chibok.
Amesema yupo tayari kuwaachia wanamgambo waliokamatwa wa Boko haram ili kupata uhuru wa wasichana waliotekwa.Lakini amesema ni vigumu
kutambua nani kiongozi katika kundi hilo baada ya kuzuka mgawanyiko katika uongozi mwaka huu.
Buhari alikuwa akizunguma pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa New York.
Kutekwa kwa wasichana hao wa shule kulisababisha kuzuka kwa kampeni ya #BringBackOurGirls, ilioungwa mkono na mkewe rais wa Marekani Michelle Obama na mwanaharakati wa Pakistani Malala Yousafzai.
Mpaka sasa ni msichana mmoja pekee wa shule aliopatikana baada ya kuzuiwa kwa miaka miwili.
Katika mizei minane iliyopita, Boko Haram imepokonywa udhibiti wa sehemu nyingi baada ya kusukumwa nyuma katika operesheni ya jeshi la nchi na mataifa jirani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni