Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka
mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na
chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia Reuters kuwa taifa la
Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za
kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.''Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni