Kampuni ya Microsoft imeshtumiwa na kundi la haki za wateja la Consumer Rights dhidi ya programu yake ya Windows 10.
Kundi hilo limesema limepokea mamia ya malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa programu hiyo .
Watumiaji wa programu hiyo wanalazimika kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na faili kupotea.
Hatahivyo
Microsoft ilitetea programu hiyo ya Windows 10 na kusisitiza kuwa
imekuwa ikitoa usaidizi kupitia mtandaoni na vilevile kwa simu.
Imeongezea kwamba itawasaidia watu kupata programu yenye manufaa na yenye usalama dhabiti, kulingana na msemaji wa kampuni hiyo.
Kundi hio limesema watumiaji wamekuwa wakilalamikia ujumbe uliokuwa
ukijitokeza kwenye tarakilishi na simu zao kila mara, kuwahimiza
kuboresha programu hiyo mbali na programu hiyo ya Windows 10 kujiweka
yenyewe bila idhini ya mtumiaji.
Pia kumekuwa na malalamiko kuhusiana na huduma mbaya kwa wateja wake,pale wanapohitaji msaada kutoka kwa kampuni hiyo.
Programu
hiyo ya windows 10 ilizinduliwa mwezi Julai mwaka 2015, na hutumika
katika tarakilishi,simu aina ya smartphone, na vifaa vya kusikilizia
sauti vya HoloLens.
22 Septemba 2016
Progamu ya Windows 10 lawamani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni