Umoja wa Mataifa umefanikiwa kufikisha misaada ya kibinadamu katika kitongoji kinachokaliwa na waasi cha Moadamiya, Damascus.
Chakula
na misaada mingine ya dharura kwa takriban watu elfu 40, ilipakuliwa
ikiwa ni ya kwanza nchini humo tangu huduma hizo kusimamishwa kutolewa,
kufuatia shambulio la mauaji lililofanywa karibu na mji wa Aleppo.Mratibu wa Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Syria Jan Egeland amesema serikali ya Syria kwa sasa inaandaa vibali zaidi.
Amemtaka Rais wa Syria Bashar al- Assad kuruhusu msafara mwingine wa malori arobaini ambayo inasubiri kuelekea Aleppo kutokea katika mpaka wa Uturuki, na kusema kuwa chakula hicho kinaisha muda wa matumizi yake siku ya Jumatatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni