Meneja wa timu ya QPR Chris Ramsey amesema asili yake ya rangi nyeusi itampa wakati mgumu kupata kazi pale atakapo ondoka katika dimba la Loftus Road.
Kocha huyo alisema kuwa meneja yeyote huhangaika kupata kazi lakini inakuwa taabu zaidi kwa mweusi.
Ramsey anaiongoza klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu baada ya kupandishwa na kushika nafasi hiyo ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Harry Redknapp kocha wa zamani wa klabu hiyo aliyebwaga manyanga Februari mwaka huu. Kabla ya kuanza kazi katika timu hiyo Chris alikaa miezi saba bila kazi baada ya kuondoka Tottenham mnamo mwezi June kabla ya kujiunga na QPR mwezi October.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni