Staa wa Bongo Movies, Mayasa Mrisho ‘Maya’, amefunguka kuwa anahisi
yeye na mwigizaji mwenzake ambaye ni mkongwe, Blandina Chagula ‘Johari’
wana gundu kwani wasanii wenzao wengi wana watoto na wengine ni
wajawazito lakini wao wapowapo tu.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Maya alisema kuwa kuna
wakati anakaa na kufikiria sana hatma yao na kuona kwamba kama
imeshindikana kuolewa basi wapate hata watoto angalau nao wajidai kama
wenzao.
“Mimi na Johari ni wasanii wakongwe sasa sijui ni gundu ama nini,
kama hatupo kwenye listi ya wale wa kuolewa basi tupate hata mtoto
mmojammoja maana mimi naona tunazidi kuzeeka kabisa kila siku inayoenda
kwa Mungu,” alisema Maya.
09 Aprili 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni