Viongozi wawili wa dini nchini Kenya wameiambia BBC kwamba wamepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Alshabaab wiki tatu tu baada ya shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa.
Viongozi hao pia kutoka Garissa wamesema baadhi ya viongozi wa dini wamepokea vitisho katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.
Wana wasiwasi kwamba serikali inawashirikisha katika vita dhidi ya wapiganaji wa Al shabaab bila kuwahakikishia usalama wao.
Viongozi hao walikuwa wakizungumza baada ya kushiriki katika mkutano wa vita dhidi ya itikadi kali pamoja na viongozi wa kisiasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni