Staa wa vichekesho kutoka Bongo Movies, Joseph Senga ‘Senga’ amefunguka kuwa busu alilompiga staa wa kike wa filamu, Kajala Masanja lilimfanya alale usingizi mnono sana ukizingatia kuwa hajawahi kubusu shavu laini kiasi hicho kwasababu warembo wengi wanazingua.
Akizungumza na GPL, Senga alisema alipata fursa hiyo ya kumpiga busu wakati wakiigiza filamu matata ya Pishu iliyoandaliwa na Kajala Entertainment, itakayoingia sokoni Mei Mosi, ambapo alisema anajikubali katika filamu hiyo ambayo anaamini itavunja watu mbavu.
“Wewewee umpige busu Kajala utashindwa kulala kweli jamani,yaani nilishtuka kumeshakucha kabisa lakini pamoja na yote mimi ni mchekeshaji ila kwa filamu ya Pishu nimeinua mikono,”
alisema Senga.
23 Aprili 2015
Senga: Busu la Kajala Lilinifanya Nilale Usingizi Mnono
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni