Staa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ adaiwa kuzua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na
kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.
Gazeti la Risasi limeripoki kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella.
Mwanahabari wa gazeti hilo aliyekuwa akikusanya matukio ukumbini humo, aliwashuhudia watu waliomzunguka Ray wakionesha hofu yao pale fulana yake ilipopanda juu na kuiacha bastola yake aliyoichomeka kwenye suruali ikionekana bila kificho ambapo zaidi walihofia mazingira ya unywaji wa pombe uliokuwepo.
“Jamani hii si hatari na ‘masanga’ haya anayogonga hapa ukimkorofisha hata kidogo tu si anaweza kukushuti bila kuwaza nini kitatokea?,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa wamekaa jirani na msanii huyo.Baadhi ya watu hao waliokuwa jirani na Ray aliyekuwa amekaa pamoja na msanii mweziye Jacob Steven ‘JB’, walionekana wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine aliyekuwa eneo hilo.Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila kupokelewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni