Staa mkongwe kutoka Bongo Movies, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amegeuka mbogo baada kuulizwa juu ya madai ya kuoa binti mdogo ambaye ni sawa na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18 akidai kuwa sheria ya dini inamruhusu kufunga ndoa wa wake wanne.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa ambalo ndilo lililokuwa la kwanza kuripoti ishu hiyo, Mzee Majuto ambaye awali alionesha kuwa na jazba alifunguka:
“Hilo suala haliwahusu wala na si jambo la ajabu kabisa kwa sababu mimi ni mwanaume wa Kiislamu, sheria ya dini inaniruhusu kuoa mke wa kwanza wa pili wa tatu hadi wanne,” alisema Majuto
“Hilo suala haliwahusu wala na si jambo la ajabu kabisa kwa sababu mimi ni mwanaume wa Kiislamu, sheria ya dini inaniruhusu kuoa mke wa kwanza wa pili wa tatu hadi wanne,” alisema Majuto
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni