15 Aprili 2015

Uchaguzi mwezi Oktoba

Uchaguzi Ujao
Mwaka huu tutambue, mwezi wa kumi ujao,
Ujao tufikirie, uchaguzi mwezi huo,
Huo mwezi tuchague, viongozi  wafaao
Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Tatu moja Oktoba, wakumbushe na wenzao
Wenzio baba na mama, familia mkaao
Mkaao kwa maraba, hata pia rafikio,
Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Haki ya Demokrasi, waruhusiwa chaguo,
Chaguo la, kutaka uwapendao,
Uwapendao upesi, uweke tiki kwa hao,
Tuchague wafaao Watanzania wenzangu.
Ukumbusho daftari, jina lako liwe kwao,
Kwao liwekwe  vizuri, idadi wajue wao,
Wao ni wa kunakili, jina lako liwe kwao,
Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Kubwa sikizeni sera, za wote wagombeao,
Chagua ‘ahadi’ bora itayoleta mafanikio,
Msende tazama sura, pia makelele yao,
Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Raisi nambari wani, utaona picha zao,
Za wabunge majimboni, zitabandikwa na wao,
Wao pia madiwani, picha ndio tegemeo,
Yuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Umri nawakumbusha, kumi na nane mwanzio,
Mwanzio ukifikisha ruhusu hadi ubaoni,
Ubaoni umeshaisha, hai haupo nao,
Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.
Nia yangu ujulisho, mwaka unaenda mbio,
Mbio ona kama kesho, na hali mambo kibao.
Kibao ya uboresho, nini sasa tegemeo,
 Tuchague wafaao, Watanzania wenzangu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728