Rapper maarufu duniani Shawn Correy Carter aka Jay Z ni kama hakuna maelewano mazuri na mke wake, Beyonce.. ishu imetajwa kuwa ni kitendo cha Jay kuwasiliana naRihanna?
Jay Z ambaye anatajwa kumiliki simu tofauti za mkononi ana simu maalum ambayo Ni Rihanna peke yake ambaye ana namba ya simu hiyo na watu walio karibu na rapa huyo na mkewe wanadai kuwa Beyonce amekerwa na kitendo hiki.
Vyanzo vya story hii vimedai kuwa Rihanna ana uhuru wa kumcheki Jay Z kwenye simu muda wowote japo mawasiliano yaliyopo kati yao yako kibiashara na kikazi zaidi.. Wanaudaku wa Marekani wanasema Beyonce hapendezwi na ukaribu huu wa Jay naRihanna.
Wanaudaku wamesema Jay Z wakati mwingine huwa anakatisha mazungumzo au shughuli yoyote anayoifanya kama ikitokea amepigiwa simu na Rihanna… kingine walichoshtukia wanasema eti story zake na Rihanna kwenye simu huwa nyingi kulikoJay akiwa anaongea na mtu mwingine.
Story nyingine zinadai kuwa Beyonce na Rihanna wamekuwa hawazungumzi kwa muda mrefu na Beyonce amekuwa akimkwepa Rihanna katika hafla tofauti zinazowakutanisha karibu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni