Kweli mitandao ya kijamii ina kazi. Ukiwa na moyo mwepesi mitandao hii inaweza kuwa sio wazo zuri sana kwako.
Leo kupitia mtandao, mwanadada Aunty Ezekiel amepata na jambo
ambalo kwa upande wetu tunaona si la kiungwana hata kidogo baada ya
jamaa mmoja kuandika maneno yasio ya kibinadamu hata kidogo kwenye picha
moja aliyoiweka mwanadada huyo ambaye ni mjamzito .
Aunty Ezekiel aliweka picha yake akiwa na Wema Sepetu ambaye hapo jana aliamua kufungua juu ya tatizo lake linalomsumbua la kutoweza kushika ujauzito,
na baada ya kuweka picha hiyo ndipo alipopatwa na dhahama hiyo baada ya
jamaa huyo kuandika kuwa anatamani aunty Ezekiel akijifungua tu afe
pamoja na mtoto wake huyo, jambo ambalo si la kibinadamu kabisa
kumuombea mtanzania mwenzako
“Yani ukijifungua naomba ufe na mimba yako maana utakachozikaa kimelaaniwa” Hayo ndio yalikuwa maneno ya kijana huyo.
Baada ya kauli hiyo Aunty Ezekiel aliamua kuandika haya yafuatayo…
“Ukiacha yote ktk Maisha naamini Duniani tunapita na kila mmoja
wetu yupo ktk safari ugumu ni kutangulia na Mwenyezi Mungu si wa kwako
wala wakwang na ndio mana kila mmoja anatimiziwa haja zake kwa nafasi
yake Nataka nikwambie tuu ww kaka uliyeandika maneno hayo kwang leo kuwa
ww ni wa Mwenyezi Mungu pia dua lako linawezekana kusikilizwa na
likasikilizwa haraka couse wala haupo peke yako ila ww ndie pekee
uliepata ujasiri wa kuandika wengine watakuwa wanaomba kwa chini ila
wote tumuombae hayo ni huyo huyo mmoja hvyo bac tumuachie yy Inshaalah
ndio anajua mwisho wa kila mmoja wetu.Furaha ni ya zamu utakapokuwa
unafurahia Umauti wang Familia yang itakuwa ikilia kwa hilo na ifikapo
kwako ww unaeniombea hilo kila kukicha ni hvyohvyo pia kwa familia
yako.Hvyo nina Aman yakutosha tu kwakuwa mm ni wakwake pia
Sikujiumba.WHN JESUS SAY YES NO BD CAN SAY NO....love u all.....”
Pole sana Aunty Ezekiel. Tunakuombe ujifungue salama.
13 Aprili 2015
Pole Aunty Ezekiel kwa hili. Msamehe bure. Ni elimu tu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni