Mchezaji
Chess mtajika amefukuzwa kutoka kwenye mashindano ya kimataifa huko
Dubai baada ya kupatikana akitumia simu ilikumshinda mpinzani wake.
Gaioz
Nigalidze kutoka Georgia huenda akapigwa marufuku ya kushiriki
mashindano yeyote ya mchezo huo kwa kipindi cha miaka mitatu iwapo
shirikisho la mchezo huo duniani litampata na hatia.Bingwa huyo wa Georgia alikuwa akichuana na Tigran Petrosian kutoka Armenia katika mkondo wa sita wa mashindano ya wazi ya mchezo huo huko Dubai.
Petrosian aliwaarifu maafisa baada ya kushuku nia halisi ya mpinzani wake kukimbia chooni kila baada ya kipindi fulani.
Kulingana na Petrosian mpinzani wake alikuwa akiingia katika choo kilekile kwa muda wa takriban dakika kumi.
Maafisa walimvizia na kumfumania alipotoka chooni .
Na baada ya upekuzi waligundua simu ya kisasa iliyokuwa imefichwa ndani ya jaa ikiwa imefungwa na karatasi.
uchunguzi wa kina ulibaini kuwa simu hiyo ilikuwa na mfumo wa mchezio huo wa kielektroniki ambao Nigalidze alikuwa akiiuliza ushauri kila baada ya mpinzani wake kumbana.
Mkurugenzi wa mashindano hayo bwana Yahya Mohamed Saleh aliiambia BBC kuwa simu hiyo ilikuwa na Mfumo wa kielektroni wa mchezo huo kwenye mtandao wake wa facebook.
Wawili hao walikuwa wakiwania tuzo la mshindi la dola elfu $12,000 (£8,000).
Shirikisho la mchezo huo la Georgia limesema kuwa limehuzunishwa mno na tukio hilo na kusema kuwa mchezaji huyo kwa kawaida huwa ni mweledi wa mchezo wake.
''hatujui kwa hakikika ni nini kilichomsibu kwani Gaioz Nigalidze huwa na ujuzi mkubwa sana wa mechi'' alisema Sofiya Nikoladze
Mchezaji huyo ameorodheshwa katika nafasi ya 400 bora duniani katika mchezo wa hess.
Hii ndiyo itakuwa mara ya kwanza kwa gwiji wa mchezo huo ama ''grandmaster'' ameripotiwa kwa shirikisho la kimataifa la mchezo huo (FIDE) kwa kuiba matokeo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni