Mahakama
moja mjini Busia, imewahukumu washukiwa watatu vifungo vya kati ya
miaka saba na kumi na tano gerezani,baada ya kuwapata na hatia ya
kumbaka na kumjeruhi msichana mmoja, aliyefahamika kama Liz.
Liz inasemekana alishambuliwa na vijana hao na kubakwa wakati alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa mazishi ya babu yake katika eneo la Busia Magharibi mwa Kenya.
Tukio hilo lilizua mjadala mkali nchini Kenya huku wanaharakati wa kijamii wakishinikiza serikai kuwachukulia washukiwa hao hatua kali.
Watatu hao walikuwa wamehukumiwa ''kufyeka nyasi katika kituo cha polisi'' na kuachiliwa huru.
Hata hivyo msichana huyo alikuwa amepooza kiwiliwili chake kuanzia kiunoni kufuatia kutupwa katika shimo ilikuficha ushahidi alipata
msaada baada ya wanaharakati wa kupigania haki za kibiniadamu kuishinikiza polisi kuchukua hatua dhidi ya polisi waliotoa hukumu hiyo nyepesi dhidi ya watu hao watatu.
Mamake Liz ameiambia BBC kuwa hatimaye haki imetendeka.
Watatu hao sasa wamepatikana na hatia ya kumjeruhi Liz na kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 Jela.
They were also found guilty of causing bodily harm and sentenced to 7 years in prison.
Harakati za kumtafutia haki msichana huyo ziligonga vichwa vya habari mwaka uliopita watu zaidi ya miklioni 2
kote duniani walipotia sahihi kampeini ya kumlazimisha Inspekta mkuu wa Polisi
kuwachukulia hatua watatu hao ambao walikuwa wamedaiwa kuwahonga maafisa polisi huko Busia Magharibi mwa Kenya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni