Kufuatia kuhusishwa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu Bilionea Lusekelo Samson Mwandenga ‘Seki’ aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita, Staa wa Bongo Movies Elizaberth Michael ‘Lulu’ amesema hana la kusema na hana tamko lolote fufuatia kifo cha Seki.
Akiongea na gazeti la Ijumaa Wikienda Juzi, lililotaka kujua taarifa za yeye kuhusishwa na bilionea huyo pamoja na mambo mengine, Lulu alijibu kwa kifupi;
Mwandishi: “Lulu kwanza tumesikia unaumwa na umelazwa, ni kweli?”
Lulu: “Siyo kweli, mimi mbona nipo tu hapa nyumbani.”
Mwandishi: “Kuna manenomaneno kuhusu kifo cha Seki, watu wanakusema vibaya mitandaoni. Je, unatoa tamko gani?”
Lulu: “Sina tamko lolote.”
Mwandishi: “Lakini ni mtu uliyekuwa unamfahamu au alikuwa mpenzi wako?”
Lulu: “Sina cha kusema mimi na sina tamko lolote.”
Gazeti hilo lilipojaribu kumbana kwa maswali zaidi kuhusiana kuwa na uhusiano na bilionea huyo, kutofanyika kwa bethidei yake na kufuta akaunti ya Instagram, Lulu hakuwa tayari kujibu lolote.
Marehemu Seki ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa madini, Arusha na Dar ameacha mke na watoto wawili.
Mwili wake ulitarajiwa kuagwa jana katika Kanisa la KKT, Wazo-Hill jijini Dar na kusafirishwa mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni