Chanzo makini kinachofahamu kwa undani kinachoendelea baina ya mastaa
hao wawili, kimelidokeza gazeti la Amani kuwa tukio hilo lilijiri
wakati wakielekea katika shughuli za mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip
Top Connection, Abdul Bonge aliyezikwa kijijini kwao Mkuyuni mkoani
humo, ambako watu wengi maarufu walihudhuria.
“Si unajua mastaa kibao walikuwepo kwenye ule msiba, basi Rose na
Shetta nao walikuwepo na wakati wa kwenda Mkuyuni, walipanda gari la
Shetta hadi Morogoro mjini ambako walichukua chumba na kulala wote hadi
kesho yake walipohudhuria mazishi na kurejea Dar es Salaam,” kilisema
chanzo hicho.
Ili kushibisha maelezo yake, mtoa habari huyo alilitumia gazeti hilo
video ya wawili hao wakiwa ndani ya gari la Shetta inayomuonyesha Rose
akiimba nyimbo mbalimbali za msanii huyo.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama uhusiano wa wawili
hao ni wa siku nyingi au umeanza hivi karibuni, ingawa gazeti hili
linafahamu kuwa Shetta ni mume wa mtu akiwa amezaa naye mtoto mmoja.
Gazeti hilo lilimtafuta Shetta na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu
yake ya mkononi na aliposomewa mashtaka, kwanza alicheka na kusema kuwa
ni kweli alikuwa msibani na alirejea Dar akiwa na Rose katika gari
lake.
“Ninachoweza kusema ni kuwa ni kweli nilimpa lifti Rose wakati
tunaenda kwenye mazishi ya Bonge. Kulikuwa na magari mengi ambayo mtu
yeyote angeweza kupata lifti na ni kweli pia tulilala Morogoro, ilikuwa
ni hoteli moja lakini kila mtu alilala chumba chake, siwezi kujihusisha
na hayo mambo, mimi nina familia,” alisema msanii huyo ambaye pia
aliwahi kutamba na kibao cha Kerewa, alichomshirikisha Diamond.
Kwa upande wake, Rose Ndauka alipoulizwa kuhusu suala hilo, kwanza
alishtuka na kuuliza zilikopatikana habari hizo kabla ya kukiri ukweli
kuwa alipanda gari la Shetta na wote kulala hoteli moja mjini Morogoro,
lakini kila mtu na chumba chake.
“Halafu nisingependa kuandikwa andikwa kila siku kwa mambo hayo,
unajua kama mimi nina mtu wangu? Andikeni halafu tutaonana mahakamani,
maana naona lengo lenu ni kuniharibia,” alisema Rose.
09 Aprili 2015
Rose Ndauka, Shetta Wadaiwa Kulala Chumba Kimoja
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni