Muigizaji maarafu wa filamu nchini Tanzania,Wema Sepetu alizomewa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kuweka picha ya mlimbwende Hamisa Obetto akiwa mjamzito na kuandika maneno ya mshangao”Jamani my mdogo umezaa.!wewe ni mwanamke sasa”.
Ujumbe huo ulizusha tafrani kwa baadhi ya watu na kumjibu Wema kwa maneno makali yenye kebehi ya
kwa nini yeye hazai anakaa kushabikia watoto wa wenzie tu.
Gumzo hilo lilifwata mkondo tofauti pale ambapo mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum
akitarajia kupata mtoto na bi.Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani wake mkubwa Wema.
Wema Sepetu aliweza kujibu tuhuma hizo kwa kusema yeye si mpanga wa yote,''ningekuwa na uwezo wa kuzaa angezaa siku nyingi ila ni Mungu ndiye anapanga'',
Alisema kuwa ''nimekuwa nikihangaika kupata mtoto usiku na mchana''
aliongezea kusema kuwa si rahisi kwa yeye kuwaambia kila kitu,kwani yeye pia ni binadamu na kuwa
''anaumia sana na maneno makali watu wanayoandika au kusema kumhusu''.
Ujumbe wa simanzi kutoka kwa muigizaji huyo ulirudiwa na baadhi ya waigizaji kama Iren Uwoya na mashabiki wengine
ukionya tabia ya watu kutoa matusi makali kwa Wema bila kuangalia upande wa pili,maana siku hizi kuna team kwenye mtandao pia zikijiita team Wema na Team Zari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni