Baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake kugombea urais kwa muhula wa
tatu.Maandamano makubwa yameendelea nchini humo na kugharimu maisha ya watu ,waandamaji hao wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi waliokuwa wakijaribu kuyadhibiti maandamano hayo.wafuasi hao wameapa kuendelea na maandamano hayo, hadi rais Nkurunzinza atakapobadili uamuzi wake wa kuwania urais kwa muhula mwingine.
Mwandishi wetu Regina Mziwanda ,amefuatilia kinachoendelea Burundi kwa sasa na amezungumza na Msemaji wa Rais wa Burundi Jervier Abayeho na kwanza amemuuliza msemaji huyo kuwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anafikiria kufanya mazungumzo na upinzani ili kuondoa mvutano unaoendelea sasa nchini humo?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni