Ndege
ya moja ya shirika la ndege la Alaska ililazimika kutua kwa dharura
huko Seattle baada ya mhudumu wa ndege kugundulika alikuwa amesahaulika
ndani ya sehemu ya kupakia mizigo ya ndege hiyo.
Rubani wa ndege hiyo alishtuliwa na mlio tofauti uliosikika ukitokea chini ya kiti chake na mara moja akaomba kutua kwa dharura.Ndege hiyo ya Alaska yenye usajili wa nambari 448, ilikuwa ikielekea Los Angeles.
Punde walipotua katika uwanja wa ndege bwana huyo aliibuka kutoka ndani ya kasha la mizigo na kudai kuwa alikuwa amesinzia.
Shirika la ndege lilitoa taarifa ya kusema kuwa bwana huyo alikuwa amepimwa na kupatikana kuwa hakuwa mlevi wala kutumia madawa yeyote.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliyokuwa na abiria 170 ilikuwa imepaa kwa dakika 14 angani.
Awali afisa anayesimamia wahudumu katika uwanja wa Seattle aliiambia shirika kuwa walikuwa wamegundua bwana huyo hayupo na wakampigia simu lakini haikuwa inapokelewa.
''Wafanyikazi wenza walidhania kuwa alikuwa amekamilisha wajibu wake na hivyo akaondoka''
Abiria mmoja Marty Collins,aliiambia runinga moja ya Seattle kuwa hawakuwa wamesikia sauti hiyo.
Shirika la ndege hilo lilisema mfanyakazi huyo aliajiriwa na Menzies Aviation na kwamba alianza kazi kumi na moja alfajiri na alipaswa kuondoka masaa 14:30 lakini alilala katika shehena ya mizigo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni