Staa alieanzia Bongo Movie na kuingia kwenye Bongo Fleva
Snura Mushi ‘Mama wa Majanga’ simu yake ya mkononi imetekwa na wajanja
wa mjini kwa kuswap na simu anazopigiwa yeye kwenda kwa mtu mwingine
ambaye hata hamjui wala hana mahusiano naye na hajui alitumia njia gani
kuiteka hajui.
“Hata sielewi mtu huyu kafanyeje hadi namba yangu kuitumia yeye, na
mbaya zaidi ni pale ambapo kilaanapobahatisha namba ya rafiki yangu
huomba atumiwe pesa nahisi lengo lake kuu ilikuwa ni kujipatia pesa kwa
njia ya utapeli na kujiita Snura,”anasema Snura.
Katika kuepuka hilo msanii huyo ameamua kuiachana namba hiyo na
anapatikana katika namba mpya ambayo anawasiliana na jamaa zake pamoja
na wateja wake wanaomhitaji katika show za muziki hivyo kwa wapenzi wake
waliokumbwa na mikasa ya tapeli huyu anawapa pole na wakiombwa fedha na
mtu huyo wasimtumie ni muongo.
14 Aprili 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni