Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa treni mpya ya abiria (Deluxe), abiria wa awali kutumia usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, wamekosa ustaarabu na kufanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa.
Akizungumza mjini Kigoma, Meneja wa treni hiyo, Jonas Afumwisye, alisema baada ya kufika Kigoma, waliifanyia ukaguzi, ndipo wakagundua kuwepo kwa uharibifu katika baadhi ya vyumba vya daraja la pili na sehemu ya daraja la tatu la treni hiyo. Alitaja moja ya maeneo yaliyoharibiwa kuwa ni pamoja na kung’olewa kwa mkono wa kupandishia na kushusha kitanda cha kati katika chumba cha daraja la pili. Mbali na kung’oa kabisa mkono huo wa kitanda, kwenye moja ya mabehewa ya daraja la tatu, abiria wameng’oa baadhi ya mapazia hatua iliyosikitisha uongozi wa Kampuni ya Reli (TRL), ambao umekusudia safari za treni hiyo ziongezeke kutoka mbili hadi tatu kwa wiki tofauti na ile ya zamani.
Nini ungependa kuwaambia waliofanya uharibifu huu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni