Waganga wa kienyeji wanaotoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania wamejitolea kumtibu Msanii
WemaSepetu aweze kupata mtoto.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya Waganga hao waliojitolea walipiga simu kwa mtandao wa Bongo Movies.com baada ya kukiri kwa nyota huyo wa filamu kwamba hawezi kupata mtoto.
Wameapa kumtibu tatizo hilo.''Wajua kuna wanawake wanaopata matatizo madogo kama kutoweza kupata mtoto licha ya kwamba kuna matabibu wanaoweza kutatua matatizo yao.
Tatizo la wema sio la kumtia wasiwasi,linaweza kutibika''walisema.
Mpatie nambari yangu ya simu na umwambie anipigiemmoja wa waganga hao alisema.
Na ili kutaka kujua vile Wema alijibu ombi hilo ,inadaiwa kuwa alikubali kusaidiwa na watabibu hao lakini kwa masharti.
''Kuna wengi zaidi mbali na waganga ambao wamejitolea kunisaidia.nina zaidi ya ujumbe 400 niliyotumiwa katika mtandao wangu wa WhatsApp huku simu nyingi zikipigwa.Ukweli ni kwamba niko tayari kupokea usaidizi huo.'',alijibu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni