Staa mrembo wa Bongo Movies, Ester Kiama, juzikati aliwatoa udenda
wanaume waliokuwa ndani ya Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi jijini Dar
baada ya kutinga akiwa amevaa kivazi cha kihasara ile mbaya.
Ester aliingia hotelini hapo akiwa amevaa shati tu na kuacha wazi
eneo la kuanzia mapajani, kitendo kilichowafanya wanaume wengi kuacha
shughuli zao na kumkodolea macho.
“Hee! Huyu ni Ester yule msanii wa filamu? Mama yangu weee, ndo’
kavaa kivazi gani kile sasa. Yaani huyu ipo siku atatembea uchi,”
alisikika akisema kijana mmoja aliyeonekana ni mfanyakazi wa hoteli
hiyo.
Hata hivyo, licha ya wanaume kumpa wakati mgumu huku wengine
wakimpigia miluzi na kumuita, yeye aliendelea na hamsini zake ambapo
alikwenda upande wa ufukweni na kujiachia zaidi.
13 Aprili 2015
Ester Awatoa Udenda Midume Hotelini
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni