Ukraine
imesema kuwa imewapoteza maafisa wake 6 wa kijeshi katika kipindi cha
saa 24 zilizopita kufuatia mashambulizi ya wapiganaji wanaotaka
kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.
Msemaji wa jeshi la Ukraine amesema kuwa kumekuwa na ufyatulianaja wa risasi usiku kucha.Mapigano yameripotiwa kuendelea viungani mwa mji wa Donetsk.
Mwandishi wa BBC aliyekuwa na waasi wanaounga mkono Urusi pamoja na wakaguzi wa Ulaya karibu na kijiji muhimu cha mji wa Mariupol alisikia milipuko na kuona makombora yakirushwa.
Mwandishi mmoja wa Urusi aliyekuwa na kundi hilo alijeruhiwa vibaya.
Awali mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain walieelezea wasiwasi uliopo kufuatia kuibuka upya
kwa mapigano mashariki mwa Ukraine hatua iliyokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Februari.
Baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya
silaha ambazo zitaondolewa ni pamoja na vifaru na bunduki nzito nzito zenye uwezo wa uharibifu mkubwa.
Pande hizo mbili zilionekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege wa Donetsk na kijiji cha Shyrokyne nje ya mji wa Mariupol.
Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni