Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya
kuona habari za mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zarinah Hassan zinapamba moto kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la project.
Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga kazi badala ya kupoteza muda.
“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki tena kushabikia mambo ya Zari na Diamond kwa sababu hayatuhusu,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni