JESHI la Polisi mkoani Simiyu, linamshikilia mkazi wa Bariadi mkoani hapa, Joyce Mganga (60), kwa kosa la kuwachoma moto wajukuu zake kwa kutumia panga la
moto.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Jonathan Shana, alisema tukio hilo lilitokea Machi 24, saa 2 usiku, bibi huyo inadaiwa kuwa alishirikiana na mtoto wake Faraja Misano (30) kuwafanyia ukatili huo.
Kamanda Shana alisema, chanzo cha watoto hao kufanyiwa ukatili huo, ni kuwatuhumu kuwa ni wezi na kudai kuwa walimchukulia baba yao mdogo (Faraja) fedha Sh. 25,000.
Watoto waliojeruhiwa ni Neema Godrey (15), na Anastazia Misano (13) ambao walikuwa wanaishi na bibi yao kutokana na baba yao mzazi kufariki.
Hata hivyo, wakati jeshi la polisi likiendelea kumsaka kijana wa bibi huyo ambaye alitoroka, bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumfikisha mahakamani.
Aidha, polisi imeitaka jamii kuacha tabia ya kuwafanyika watoto ukatili kwa kuwa watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakati huo huo jeshi hilo limewakamata Juma Kulwa (25), Juma Makulwa (33) na Maka Sibusa, wakazi wa kijiji cha Kadoto, wilayani Maswa kwa kosa la kumkata mapanga Mwalu Ngusa (25) kwa kumtuhumu kuwaroga watoto wa jirani yake.
01 Aprili 2017
Bibi wa miaka 60 kwa tuhuma za kuwachoma wajukuu wake
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni