RAPA anayetamba na ngoma ya Sweet Mangi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefungukia maisha yake ya kimapenzi na
kusema hawezi kumweka wazi mpenzi wake kwa kuwa maisha hayo ni kama maigizo.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Nikki amesema maisha ya kuweka mambo binafsi hadharani yanamfanya aone yupo katika maisha bandia kwa kuwa eneo kubwa huwa ni maigizo.
“Siwezi kuweka wazi maisha yangu na mpenzi wangu hadharani, mimi napenda kuishi kiuhalisia, napenda kupenda na kupendwa pia, maigizo siyo kariba yangu, kuna watu wanatengeneza pesa ndefu kwa kugeuza uhusiano wao kuwa biashara, hao ni wao ila mimi siwezi,” alisema Nikki wa Pili.
01 Aprili 2017
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni