Mwanamke mmoja nchini Australia mwenye umri wa miaka 55 amenusurika kifo jioni ya jana February 23, 2018 baada ya kushambuliwa na papa wakati anaogelea baharini katika eneo la Sydney Kusini-Mashariki.
Inaaminika kuwa papa huyo alikuwa na urefu wa kati ya mita 2.7 hadi 3.2. Mwanamke huyo alikimbizwa hospitali ya St George kupatiwa matibabu ambapo alikuwa amejeruhiwa kwenye mguu wake wa kulia.
Wakazi mbalimbali wa eneo hilo waliliambia shirika la utangazaji nchini Australia la ABCkuwa tukio hilo limewashtua kwani halijatokea kipindi cha zaidi ya miaka 25 hivyo ni la ajabu.
Mwanamke huyo amefanyiwa upasuaji na afya yake imeanza kuimarika
24 Februari 2018
Mwanamke anusurika kifo kwa kushambuliwa na samaki aina ya PAPA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni