Maelfu ya watu wamekusanyika nchini
Afrika Kusini kwa mazishi ya mwanaharakati wa kampeni dhidi ya
ubaguzi
wa rangi nchini humo Winnie Madikizela-Mandela.Maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Soweto karibu na mji mkuu wa Johannesburg ambapo Winnie Mandela anazikwa.
Jeneza lake lilifunikwa na bendera ya taifa hilo na rais wa Afrika Kusini alisoma kumbukumbu ya marehemu.
- Winnie Mandela afariki dunia Afrika Kusini
- Kwa Picha: Maisha ya Winnie Mandela
- Chama cha ANC cha Afrika Kusini kumchagua kiongozi mpya
Bi Madikizila Mandela alipongezwa kwa mchango wake wakati wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi nchini Afriika Kusini.
Lakini baadaye aliipuuzwa na wanasiasa wakuu kwa kuunga mkono mauaji ya majasusi wa serikali.
Mwana wa Madikizela Mandela , Zenani Mandela Dlamini aliwashutumu wale aliotaja walikuwa na kampeni mbaya ya kumchafulia jina mamake na kumtenga kabla ya kumsafishia jina baada ya kifo chake.
''Inakera kuona vile walivyomchukulia wakati wa maisha yake, wakijua vile walivyomuumiza. Wanajua ni kwa nini waliamua kuanza kusema ukweli baada ya kifo chake'', alisema Bi Mandela Dlamini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni