IMEANDIKWA: Mungu akasema,
“Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;”.... » MWANZO 1:29
KIPEKEE; Matunda na majani ya mti wa mpera vina vitamini C kwa wingi, huku ikiambatana na madini ya potassium kwa asilimia chache 15%.
Kutokana na sifa tajwa, basi fahamu kuwa iwapo ukikosa tunda la pera unaweza kutumia majani yake kama m’badala; ili kujipatia faida za asili, zinazotokana na mpera kwa faida ya afya ya mwili wako. Nami nimekuja nikudokeze japo kwa ufupi, faida za matunda na majani ya mpera; iwapo utabarikiwa kuwa nayo karibu.
Kutokana na sifa ya vitamini C & madini tajwa yaliyomo ndani yake, tunda la pera pamoja na majani yake; yanasaidia sana ustawi na uimara wa mifupa ya mwili wako, huku yakiwa pia na uwezo/neema ya kuchochea pia kinga ya mwili
Ila tambua katika tunda lake, utapata madini ya potassium zaidi kuliko vitamini C; hii ni kwa sababu ya mbegu za mpera, zimebeba madini husika kwa asilimia kubwa kuliko vitamini C. Ni
majani yake ndiyo yaliyobeba VITAMINI C zaidi.
JE! UMEWAHI KUTUMIA MAJANI YA MPERA KAMA M’BADALA YA MAJANI YA CHAI !?
Majani ya mpera ukiyafanya kuwa kiungo kikuu cha chai, basi utakuwa umeji-tengenezea dawa kwa jina la chai; inayo shughulika na kuondoa mafuta yanayoganda mwilini (cholesterol), bila kusahau na kusafisha sumu zinginezo mwilini.
FAIDA ZA ZIADA NI:
~Inaimarisha afya ya ngozi.
~Inaponya maumivu ya tumbo na kuharisha.
~Inasaidia kuweka uwiano wa sukari mwilini.
~Inaboresha afya ya uoni kwenye macho (B3).
~Inasaidia kupunguza uzito mkubwa (obesity).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni