11 Januari 2016

Mgawanyiko wanukia kanisa la Kianglikana

 
Mgawanyiko katika kanisa la Kianglikana kuhusu suala la mapenzi ya jinsia moja halitakuwa janga bali itakuwa ni kufeli. Hii ni kwa mujibu wa askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa kanisa hilo Welby, anasema kuwa anataka kuwepo uwiano lakini hiyo ina maana ya kupata njia za kutofautiana kwa nja iliyo nzuri.
Kanisa la kianglikana lina waumini karibu millioni 80 kote duniani katika zaidi ya nchi 160, wengi wakiwa wanamuona askofu Welby kama uongozi wa kanisa hio.
 
Image caption Wengi wanamuona Welby kama uongozi wa kanisa
Watunza sera wanasema kuwa kanisa la kianglikana ni lazima lishikilie tamaduni zake.
Lakini maoni ya nchi nyingi za Afrika ambapo mapenzi ya jinsia moja ni makosa, hufanya mambo kuwa magumu kwa kanisa hilo kuwa na msimamo mmoja, huku makanisa mengi yakipinga vikali ndoa za jinsia moja na mskofu shoga.
Kuna wasi wasi kuwa waakilishi kutoka nchi za Afrika huenda wakaondoka kwenye mkutano wa Canterbury.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728