Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.
Budi Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye kisiwa na kizingirwe na mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda wanadamu, kwani hawawezi kuhongwa.
Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo kutafuta mamba wakali zaidi.
Indonesia ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu hiyo kwa miaka mine 2013.
"Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo.
"Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi waruhusu washukiwa watoroke.”
Mpango huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo nab ado haijaamuliwa gereza hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa, shirika la habari la AFP limesema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni