14 Novemba 2015

Maombolezo na hali ya hatari Ufaransa

Kundi la wapiganaji la Islamic State limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Wanajeshi wanalinda mji wa ParisRais Hollande ameelezea mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi.
Image copyright PA
Image caption Shambulizi Paris
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.

Image copyright AP
Image caption Usalama waimarishwa Paris
Wakuu wanasema paspoti ya Syria ilionekana karibu na mwili moja.
Watu kama 80 walikufa katika tamasha la muziki wa roki - ambako washambuliaji waliwakabili mateka wao na kuwapiga risasi.
Image copyright EPA
Image caption Maafisa wa polisi waimarisha doria za usalama Paris
Hapo awali, watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi nyingi dhidi ya mikahawa iliyo karibu na kusababisha hasara kubwa.
Wengine waliripua mabomu karibu na uwanja wa michezo wa taifa, ambako Ufaransa ikicheza mechi ya kandanda na Ujerumani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728