Shirika la Umoja wa Mataifa linasema watu 40,000 wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya maafisa wa usalama kutoka maeneo mawili.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema watu 30 wameuawa katika makabiliano hayo yanayoendelea katika maeneo ya Galkayo, eneo lililoko katikati ya Somalia na Puntland Kaskazini .
Kumekuwepo mapigano ya muda mrefu ya kiukoo katika maeneo hayo mawili.
Umoja wa mataifa unasema wakimbizi hao wanahitaji vyakula misaada ya matibabu, maji na huduma za usafi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni