16 Desemba 2015

Fabregas: Wachezaji wacheze sawa na mishahara

ChelseaImage copyrightEPA
Image captionChelsea wamo nambari 16 ligini wakiwa na alama 15
Kiungo wa kati wa Chelsea amesema wachezaji wa Chelsea wanaolipwa mishahara mikubwa wanafaa kucheza kama wachezaji nyota.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Premia wamedorora sana msimu huu na wamo nafasi moja juu ya eneo la kushushwa daraja baada ya kushindwa Jumatatu ugenini Leicester.
Baada ya mechi hiyo, meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema juhudi zake zilisalitiwa na baadhi ya wachezaji.
“Ikiwa wewe ni mchezaji nyota, na unalipwa kama mchezaji nyota, unafaa kucheza kama mchezaji nyota na kujibeba kama mchezaji nyota,” kiungo wa Uhispania Fabregas amesema.
“Sisemi kwamba huwezi kuwa na msimu mbaya na mechi mbaya lakini mtazamo lazima uwe ule ule.
“Lazima tusalie kucheza vyema mechi zetu, na tabia yetu inafaa kuwa tofauti na tunayoona sana kwa kila mchezaji wa Chelsea.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728