Mbwa ambaye anayefugwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwauma wageni wawili, akiwemo mbunge, katika hafla ya kidini.
Kisa hicho kilitokea katika hafla ya kuwasha michumaa kuadhimisha sikukuu ya Kiyahudi ya Hannukah nyumbani kwa Bw Netanyahu.
Mbunge huyo Sharren Haskel na mume wa Tzipi Hotovely, naibu waziri wa mashauri ya kigeni, hawakuumia sana.
Bw Netanyahu alimchukua mbwa huyo kwa jina Kaiya kutoka kwa kituo cha kuwaokoa wanyama waliotelekezwa mapema mwaka huu.
Waziri mkuu huyo alipakia kwenye Twitter picha yake akiwa na mbwa huyo wa umri wa miaka 10 mwezi Agosti.
"Ukitaka mbwa, tafuta mbwa aliyekomaa kutoka kituo cha kuwaokoa wanyama. Hutajuta,” aliandika.
Kaiya amekutana na wageni mashuhuri akiwemo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John Kerry.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni