01 Desemba 2015

Xi Jinping ziarani Zimbabwe

Image copyrightAP
Image captionXi Jinping akitumbuizwa nchini Zimbabwe
Rais wa China Xi Jinping yuko nchini Zimbabwe katika ziara ya siku mbili inayolenga kujenga mahusiano na Zimbabwe.

Rais huyo anatarajiwa kufanya mkutano wa moja kwa moja na mwenyeji wake hii leo rais Robert Mugabe.
Jinping ndiye rais wa kwanza wa China kufanya ziara nchini Zimbabwe katika kipindi cha takriban miaka 20
Image captionXi akikagua gwaride la heshima Zimbabwe
Rais huyo wa China amepokelewa kwa shangwe na taadhima katika uwanja wa ndege wa kimataifa na raia waliojawa na furaha wakiongozwa na rais Mugabe.
Maafisa nchini Zimbabwe wanatarajia kuwa makubaliano kadha yenye thamani ya mabilioni ya pesa yatatiwa sahihi yakiwemo mikataba ya ujenzi wa miundo msingi, kilimo na vilevile katika sekta ya uchukuzi.
Image captionMaafisa nchini Zimbabwe wanatarajia kuwa makubaliano kadha yenye thamani ya mabilioni ya pesa
Lakini wanasiasa wa upinzani wamepuuzilia mbali ziara hiyo wakisema kuwa Uchina, haitawekeza hadi chama tawala cha ZANU-PF kiamue ni nani mrithi wa Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka tisini na moja.
Uwekezaji wa China barani Afrika ulidorora kwa zaidi ya asilimia 40 miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kutokana ukuaji mdogo wa uchumi nchini humo..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728