Je umewahi kutuma picha za utupu kwa mpenzi wako ?
Je ulimshawishi akutumie ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi tahadhari.
Kwa mara ya kwanza mahakama imeamuru kulipwa kwa fidia na msichana mmoja ambaye alishurutishwa kutuma picha za utupu kupitia mtandao wa kijamii.
Hii ni kufuatia kesi ambapo msichana mmoja alishawishiwa kutuma picha zake za uchi kwenda kwa mwalimu wake.
Sasa inamaanisha kuwa yeyote ambaye atadhulumiwa kwa kushurutishwa kutuma au kupokea ujumbe unaohusu ngono au picha na kuathiriwa kisaikolojia kutokana na hilo anaweza kudai fidia.
BBC ilipata fursa ya kuzungumza na muathiriwa katika kesi ambapo muathiriwa mwenyewe hawezi kutajwa jina.
Muathiriwa anasema kuwa akiwa bado kijana alifanya urafiki na mwalimu katika shule mpya.
Mwalimu hiyo William Whillock alikuwa naibu mkuu katika kitengo cha kulinda watoto katika shule hiyo na alikuwa na umri wa miaka 50 hivi wakati huo.
"Alikwa kama babangu," msichana huyo alisema.
"Alikuwa akiniambia kuwa kama nina shida yoyote niwe nikimpigia simu.''
Muathiriwa anasema kuwa akiwa shule, alikuwa akienda kwa ofisi yake kumueleza shida alizo nazo nyumbani.
Wakati uhusiano kati yao ulipokua zaidi mambo yakaanza kwenda mrama.
Anasema kuwa bwana Whillock angeweza kupigia simu au kumtumia ujumbe usiku wa manane akitaka amtumia picha zake za utupu.
Akiwa na umri wa miaka kumi na nane muathiriwa alimtumia mwalimu picha zaidi akiwa nusu uchi.
Licha ya kumuambia atoe picha hizo kwa simu yake, simu yake iligunduliwa na mwalimu mwingine shuleni.
Bwana Whillock alikamatwa mbele ya wanafunzi na kukiri kumiliki picha za mwanafunzi alipofikishwa mahakamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni