20 Desemba 2015

Tishio la 'Bomu' lalazimu ndege ya Ufaransa kutua Kenya

Image copyright AP
Image caption Wataalamu hao wanatoka kikosi cha jeshi la wanamaji wa Kenya na idara ya polisi wa upelelezi.
Ndege moja ya abiria ya Air France Boeing 777 AF463, inayohudumu kati ya Mauritius na Paris imelazimika kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mombasa - Kenya baada ya kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu kupatikana ndani ya choo cha ndege hiyo.

Mhudumu mmoja wa ndege hiyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho ndipo shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kamanda mkuu wa polisi nchini Kenya Jenerali Joseph Boinnet, amesema kuwa ndege hiyo iliyokuwa njiani kuelekea Paris Ufaransa ikiwa na abiria 473 na wahudumu 14 ilitua salama na abiria wote kuokolewa.
Image copyright Reuters
Image caption 'Bomu' yasababisha ndege ya Ufaransa kutua Kenya
Ndege hiyo inasemekana kutua saa sita usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshila wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Habari za hivi punde zinasema kuwa maafisa wa upelelezi wanasemekana kuwa wamewatambua washukiwa wawili abiria wa ndege hiyo.
Shirika linalosimamia viwanja vya ndege nchini Kenya linasema kuwa kifaa hicho kimeondolewa ndani ya ndege hiyo.
Shughuli za kawaida za usafiri zimerejea katika uwanja huo wa ndege baada ya kusitishwa ilikukabiliana na tishio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728