Waziri wa ulinzi nchini marekani Ash Carter anasema kuwa kikosi maalum cha jeshi la marekani nchini Iraq kitatumwa kuendesha oparesheni kadha dhidi ya Islamic State nchini Syria.
Bwana Carter aliiambia kamati ya bunge la Congress mjini Washington kuwa kikosi hicho kitafanya mashambulazi, kitawakomboa mateka na kuwakamata viongozi wa Islamic State.
Amesema kwa kwa sasa kuna fursa kubwa ya kuwatenganisha wanamgambo wa Islamic State walioko nchini Iraq kutoka wale walio nchini Syria.
Mwezi Oktoba marekani ilitangaza kuwa itatuma hadi wanajeshi 50 maaalum kwenda kaskazini mwa Syria kama washauri kwa vikosi vya waasi wa Kurdi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni