Shule zote za uma katika jimbo Los Angeles Marekani zimefungwa mara moja kufuatia tishio la usalama.
Tangazo hilo lilitolewa na muungano wa wakuu wa shule zote za umma unaathiri takriban shule 1,000.
Takriban wanafunzi laki 700,000 walilazimika kurejea makwao baada ya tishio ambalo kufikia sasa halijatangazwa wazi kupokewa na maafisa wa Polisi.
Yamkini ujumbe wa kuwatahadharisha umma ulipatikana kwa njia ya kielektroniki na hivyo ikawalazimu kuamuru wanafunzi wote waondoke ilikufanikisha shughuli ya kutafuta na kusaka tishio lililoko.
Tahadhari hiyo ya umma imetokea wiki mbili tu baada ya mauaji ya watu 14 katika kituo cha San Bernardino.
Watu hao walipigwa risasi na mume na mkewe ambao wanashukiwa kuwa walishawishiwa na waislamu wenye itikadi kali ughaibuni.
Polisi tayari wameanza kupekua maeneo yanayoshukiwa kuwa na hatari na wanasema kuwa shule zote zitasalia zimefungwa hadi tishio hilo litakalo ondolewa.
Afisa anayesimamia usalama wa shule za umma Steven Zipperman, amesema kuwa idara hiyo ilipokea tishio kwa njia ya kielektroniki mapema hii leo ndio sababu wakaamuru shule zikafungwa.
''tumeamua kufunga shule hadi pale tutakapobaini kuwa ni salama''
Mmoja wa maafisa wakuu usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema kuwa tishio hilo lilipokewa kupitia barua meme iliyotumwa kwa mmoja wa maafisa wanaosimamia shule Los Angeles kutoka ughaibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni