Utafiti uliofanyiwa afya ya viongozi wa mataifa mbalimbali umebaini huwa wanazeeka haraka na kupoteza miaka mitatu katika muda wao wa kuishi kwa sababu ya uongozi.
Watafiti walichunguza viongozi 279 kutoka mataifa 17, wakichunguza marais na mawaziri wakuu. Miongoni mwa viongozi waliochunguzwa ni kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani na Marekani.
Waliangalia umri wa kufariki kwa viongozi hao wakilinganisha na umri ambao wapinzani wao ambao waliwashinda uchaguzini walifariki wakiwa nao. Muda wao wa kuishi ulishuka kwa miaka mitatu ukilinganisha na wenzao wa umri na jinsia sawa, ambao hawakuwa uongozini.
Madaktari hao walisema mfadhaiko na shinikizo kutokana na uongozi viliathiri sana afya ya viongozi hao.
“Kupoteza miaka kadha ni jambo kubwa sana,” alisema Dkt Anupam Jena kutoka chuo cha matibabu cha Harvard Medical School, ambaye alikuwa mtafiti mkuu katika utafiti huo.
“Labda viongozi walihisi majukumu ya kitaifa yalikuwa na haja zaidi kuliko kula vyema na kufanya mazoezi,” alisema, akiongeza kuwa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alikiri kwamba huenda aliishia kula vyakula visivyofaa kutokana na mfadhaiko.
“Labda, kama ulimwengu ungelikuwa na amali, mtindo wake wa maisha ungelikuwa tofauti,” alisema Dkt Jena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni