Taarifa kutoka Zanzibar zinasema boti ya Royal Express iliyokuwa imebeba abiria 367 ikitokea Unguja kuelekea kisiwa cha Pemba imeshika moto ikiwa njiani baada ya injini yake moja kupata
hitilafu.
Meli hiyo ambayo ilikuwa imebeba abiria 300 watu wazima na watoto 67, inaelezwa chanzo cha moto huo inadawa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mashine na Boti hiyo. Taarifa zinasema hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo.
Meli hiyo iliondoka bandari ya Zanzibar saa moja asubuhi kuelekea Kisiwani Pemba ambapo khitilafu hiyo imetokea saa 3:30 kabla ya kufika katika bandari ya Mkoani Pemba ambapo Meli ya Serengeti iliyokuwa karibu ilikwenda haraka kuisaidia na kuwaokoa watu na mali zao na kuikokota hadi bandari ya Pemba.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Suleiman Masoud Makame, alisema walipokea taarifa hiyo kutoka kwa manahodha wa meli hiyo kuwa imezimika injini lakini waliwasiliana na manahodha wa meli ya Serengeti na kwenda kuivuta kwa kushirikiana na meli ya uokozi wa kikosi cha KMKM.
Aidha, alisema kuwa abiria wote waliokuwemo katika meli hiyo wapo salama na hakuna abiria alieathirika katika tukio hilo.
Sambamba na hayo, alisema Mamlaka tayari imemsafirisha Mkaguzi wa meli na ameelekea katika kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kuangalia hali ya chombo hicho.
Sambamba na hayo, alisema Mamlaka tayari imemsafirisha Mkaguzi wa meli na ameelekea katika kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kuangalia hali ya chombo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni