10 Desemba 2015

Mchezaji wa timu ya taifa Honduras auawa kwa risasi


PeraltaImage copyrightAP
Image captionPeralta amewahi kuchezea klabu ya Rangers ya Scotland

Mchezaji wa timu ya taifa Honduras Arnold Peralta amepigwa risasi akiwa likizoni mji wake wa kuzaliwa wa La Ceiba.
Aliuawa katika maegesho ya magari katika mji huo, ambao unapatikana katika pwani ya taifa hilo.
Kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 26, ambaye amekuwa akichezea klabu ya Olimpia, katika mji mkuu Tegucigalpa, alichezea klabu ya Rangers ya Scotland hadi Januari.
Visa vya watu kupigwa risasi Honduras huwa juu sana na taifa hilo lina mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani.
Mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la soka la Honduras Osman Madrid, alisema mauaji hayo ni ya kusikitisha na kwamba taifa hilo linaomboleza.
Haijabainika nini kilichosababisha mauaji hayo lakini polisi wanasema hakikuwa kisa cha wizi kwani hakuna kitu chochote kilichoibiwa.

PeraltaImage copyrightReuters
Image captionPeralta aichezea Honduras mechi za kufuzu Kombe la Dunia Brazil

Aliwakilisha Honduras katika Michezo ya Olimpiki 2012 jijini London lakini hakuweza kucheza Kombe la Dunia Brazil mwaka 2014 kutokana na jeraha.
Alitarajiwa kuchezea timu ya taifa mechi ya kirafiki dhidi ya Cuba wiki ijayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728