Kikosi bora cha wachezaji kumi na moja kilichocheza hatua ya makundi ya michuno ya klabu bingwa ulaya kimetangazwa na Uefa.
Washambulia Cristiano Ronaldo, wa Real Madrid,Hulk anayekipiga na klabu ya Zenit St Petersburg's pamoja na Thomas Muller wa Bayern Munich ndio wanaongoza safu ya ushambuliaji kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.
Ligi Kuu England imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa.
Mabingwa Watetezi wa kombe la klabu bingwa ulaya Barcelona, hawatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji.
Kikosi kamili ni:
Kipa ni Kevin Trapp (Paris Saint-Germain
Mabeki ni kulia: Andrea Barzagli (Juventus)Thiago Silva (Paris Saint-Germain)Diego Godin (Atletico Madrid) David Alaba (Bayern Munich)
Viungo ni Sven Kums (Gent) Willian (Chelsea) Raheem Sterling (Manchester City)
Washambuliaji ni Thomas Muller (Bayern Munich) Hulk (Zenit St Petersburg) Cristiano Ronaldo (Real Madrid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni