Mahakama moja nchini Australia imepiga marufuku uuzaji wa dawa ya kichwa iitwayo Nurofen.
Mahakama hiyo inasema kuwa kampuni inayotengeneza dawa hiyo iliwahadaa wateja kuwa inatibu maumivu sugu ya kichwa ilihali uchunguzi umebaini kuwa dawa hiyo ya Nurofen hainauwezo wowote zaidi ya dawa za kawaida .
Uchunguzi pia umewapata na hatia ya kuiza dawa hiyo kwa bei maradufu ya dawa za kawaida za kupunguza maumivu ya kichwa.
Kampuni inayotengeneza dawa hiyo ya Reckitt Benckiser imejitetea ikisema kuwa kesi hiyo inahusu Australia pekee wala haiathiri masoko mengine kote duniani.
Reckitt Benckiser imesema itatii amri ya mahakama hiyo ya Australia.
Kampuni hiyo vilevile imekanusha kuwa ilikusudia kuwahadaa wateja wake.
Mahakama imeitaka iondoe madawa hayo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Madawa hayo,Nurofen Back Pain, Nurofen Period Pain, Nurofen Migraine Pain na Nurofen Tension Headache.
Uchunguzi wa tume inayodhibiti ubora wa bidhaa inasema iligundua kiungo cha 'ibuprofen lysine 342mg' kilichodaiwa kuwa maalum katika madawa hayo haikupatikana.
Reckitt Benckiser hutengeneza madawa kama Nurofen, Dettol na Harpic, miongoni mwa madawa mengine
Kampuni hiyo imeamrisha iondoe matangazo hayo ya uongo na kuweka matangazo sahihi,aidha wameamrishwa kulipa gharama ya kesi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni